03 December 2013

ZITTO AKATISHA ZIARA YA SLAA


  • CHADEMA KIGOMA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU

  • HOFU YA KUTOKEA VURUGU YATANDA MAJIMBONI 
Na Mwajabu Kigaza, Kigoma
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Kigoma, kimesitisha ziara ya Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa, Dkt. Wilbrod Slaa, ambayo ilipangwa kufanyika mkoani humo kuanzia Desemba 5 hadi 13 mwaka huu, kutokana na hofu ya usalama miongoni mwa wanachama wake.


Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Jafari Kasisiko, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, usalama katika baadhi ya majimbo mkoani humo ni mdogo sana.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameona ni bora ziara hiyo isitishwe kwanza ili kuepusha machafuko yaliyoandaliwa na wanachama dhidi ya Dkt. Slaa kama atafika mkoani humo.

“Uamuzi wa kusitisha ziara hii umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Uongozi mkoani hapa kilichofanyika Desemba Mosi, mwaka huu na kushirikisha viongozi wa majimbo mengine.

“Majimbo haya ni Kigoma Mjini, Kaskazini na Kusini ambao kwa pamoja walielezea uwepo wa njama za kuhujumu ziara hii ili kumdhalilisha Dkt. Slaa,” alisema.

Aliyataja majimbo yaliyodaiwa kuchafuka kisiasa kutokana na maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA kumvua nyadhifa za uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Bw. Zitto Kabwe kuwa ni Kigoma Mjini, Kaskazini na Kusini, wakati ambapo majimbo ya Buhigwe, Kasulu, Muhambwe na Buyungu pia hali ya usalama imedaiwa kuwa ya mashaka.

Akizungumzia msimamo wa chama hicho mkoani humo kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu kumvua uongozi Bw. Kabwe kwa madai ya kutaka kukisaliti chama, alisema kikao hicho kilikuwa halali.

“Hatua zote za kumvua uongozi Bw. Kabwe na wenzake Dkt. Kitila Mkumbo na Bw. Samson Mwigamba, zilifuatwa sasa kama anadhani ameonewa, ana haki ya kukata rufaa Baraza Kuu.

“Ziara ya Dkt. Slaa hapa Kigoma, haina uhusiano na maamuzi ya Kamati Kuu kwani ilipangwa muda mrefu na kusitishwa kutokana na vikao vya Kamati Kuu, lengo la ziara hii ni maandalizi ya uchaguzi ujao ngazi za chini,” alisema.

Aliwataka baadhi ya wanachama wanaoendesha vitendo vya vurugu na kuhujumu miundombinu ya chama kuacha kufanya hivyo kwani ni kinyume cha maelekezo ya chama kwani palipo na vurugu hakuna haki.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho kutoka majimbo yaliyotajwa kuwa na vurugu, walikutana Mjini Kigoma katika moja ya kumbi za mikutano kupinga ujio wa Dkt. Slaa, Desemba 5 mwaka huu.

Akisoma tamko la wanachama hao, Fanuel Sindika alisema wameikataa ziara hiyo kwa sababu CHADEMA kimekuwa kikiwaonea baadhi ya viongozi hasa kutoka mikoa ya Magharibi na wapo tayari kufanya vurugu ili kumdhalilisha kiongozi huyo.

Alisema hawakubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Kamati Kuu dhidi ya Bw. Kabwe ambayo hayajazingatia haki kwa mujibu wa katiba.

Aliongeza kuwa, kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa na mgogoro unaotokana na hofu ya madaraka katika nafasi ya Mwenyekiti wa chama ambayo inadaiwa kuwaniwa na Bw. Kabwe akisaidiwa na rafiki zake kwenye kampeni ili kuhakikisha anashinda kiti hicho.

Hivi karibuni, baadhi ya vijana kutoka Tawi la Mwandiga, Jimbo la Kigoma Kaskazini, walifanya maandamano ya pikipiki na kuburuza bendera barabarani, kuchoma kadi, bendera na kuvunja bango la Tawi la Msingi katika kijiji hicho









6 comments:

  1. KIGOMA MSIKILIZENI HUYO SLAA LA SIVYO MTAONEKANA WABABAISHAJI AU MNATUMIKA. ADUI UKIMKIMBIA HUTAMJUA KAMA YUKO JUU YAKO HUTAWEZA KUJUA MBINU ZAKE. NI UJUA TU KUZUIA SLAA ASITEMBELEE KIGOMA KITU KINACHOKOMAZA WATU KUSEMA WATU WANATUMIKA ILI TATIZO LIENDELEE KUWEPO.

    ReplyDelete
  2. kwa wenye uelewa haihitaji darasa ili kuyafahamu haya, na kakuna kinachoweza kueleweka bila maelezo namajadilianona pamoja, poleni sana wana kigoma kwa kukosa haki ya taarifa.

    ReplyDelete
  3. JAMAN WATU WA KG KUWENI WAELEWA MSIKILIZENI MWENYEKITI WA CHADEMA NDIPO MTAELEWA UTATA UKO WAPI HAPAITAJI ELIMU YOYOTE NI MASIKIO YENU TU

    ReplyDelete
  4. Wewe nichizi kama kama slaa wako, mtaishia hapo hapo nachuki zenu wala hamuwezi kushinda na KG mkifika mnaliwa Live

    ReplyDelete
  5. endeleni kuvua dagaa na huyo zitto wenu amieni ccm basi kama anataka

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndo maana mnavua dagaa angali wenzenu tunavua samaki

      Delete